Michezo

Deal is done: Sanchez kufanyiwa vipimo jioni ya leo

Klabu ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Alexis Sanchez kutokea Arsenal na kutarajiwa kufanyiwa vipimo jioni ya leo katika viunga vya uwanja wa mazoezi wa United wa  Carrington.

Dili ambalo pia linamuhusisha Henrikh Mkhitaryan ambaye tayari kila kitu kipo sawa na  Sanchez tayari ameshaanza safari ya kwenda Kusini mwa jiji la Manchester kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya leo siku ya Jumamosi huku akitarajiwa kupokea mshahara wa paundi  450,000 kwa wiki.

Timu nzima ya watabibu wa United walikuwa na kikosi huko Turf Moor kwaajili ya mechi yao lakini wanampango wa kukutana na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile baada ya mchezo huo.

Ingawa mpaka sasa timu nzima iliyosimamia zoezi hilo haijazungumza chochote meneja wa kikosi hicho, Jose Mourinho akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wao dhidi ya Burnley  amesema watu watarajie hivi karibuni ujio wa mchezaji huyo.

“Watarajie hivi karibuni, kama hautofanikiwa basi hautokuwepo tena usajili huo, nafahamu watu wangu hufanya mambo kwa uhakika ninahakika watafanikiwa katika zoezi hili,” amesema Mourinho akijibu maswali  ya waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Burnley.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents