Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Dear Harmorapa, Acha Maneno Weka Muziki!

Harmorapa kwa sasa siyo jina geni tena katika masikio ya mashabiki wa muziki na burudani Tanzania, japo kutokueleweka kasi ya kupenya katika kipindi kifupi.

Rapper huyo kwa sasa amekuwa machachari huku akiteka vichwa vya habari kila kukicha, huku akiendelea kujitengenezea fan base.

Napenda kuzungumzia jinsi harmorapa huenda akapotea, endapo ataendelea kufanya hiki anchokifanya sasa hivi, ingawa ni dhahiri ana watu wenye nguvu ya fedha nyuma yake na upeo mkubwa wa tasnia ya muziki akiwemo God Father wa muziki hapa nchini P-Funk Majani.

‘ACHA MANENO WEKA MUZIKI’ ni moja ya mashairi ambayo nayakumbuka katika wimbo wa Darassa ‘Muziki’, na nimeamua kuutumia mstari huo kusema na Harmorapa.Tangu mwanzoni, tumemtazama katika hatua ya mapinduzi katika sanaa Tanzania, kwa jinsi alivyoweza kucheza na mitandao ya kijamii kujipatia umaarufu zaidi kila kukicha, huku akisahau kuonyesha zaidi uwezo wake na kipaji chake kwa mashabiki kupitia sanaa. Hamorapa ameshindwa kuwaondoa shaka wale ambao bado hawaamini katika uwezo wake kimuziki.

Binafsi, ninaamini kijana huyu ana kipaji kikubwa na mengi ya kushare na mashabiki wake, hasa baada ya kuusikia wimbo wake ‘Kiboko ya Mabishoo’. Kuna kitu kipya nimekiona ndani ya sanaa yake na hivyo natamani afike mbali zaidi. Kikubwa zaidi ninachomshauri, apunguze maneno mengi ya nguoni kwa wasanii wenzake, kwani ipo siku atahitaji msaada au ushirikiano kutoka kwao, hata kama kwa theluthi moja.

Hakika muda ni mali, na mashabiki wanatamani kuyasikilizisha mashairi na mistari yako. kwa hiyo, Hamo, acha maneno, weka muziki!

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW