Michezo

Del Potro bingwa mpya wa michuano ya Indian Wells

Mchezaji tennis raia wa Argentina, Juan Martin del Potro hapo jana siku ya Jumapili amefanikiwa kunyakuwa taji la michuano ya wazi ya BNP Paribas Indian Wells baada ya kumfunga, Roger Federer.

Del Potro maarufu kama Delpo amefanikiwa kumfunga mchezaji huyo namba moja kwa viwango vya tennis duniani,Roger Federer kwa jumla ya seti 6-4 6-7 (8-10) 7-6 (7-2) na kutwaa taji hilo la BNP Paribas.

Baada ya ushindi huo, Del Potro amekiambia chombo cha sky sports kuwa hajaamini kama angetwaa taji hilo mpaka pale alipotangazwa.

Nilikuwa sijiamini mpaka pale nilipotangazwa, nivigumu hata kuzungumzia hilo imekuwa kama ndoto kwangu.

Baada ya matatizo yote, baada ya upasuaji wangu wote na majeraha yaliyokuwa yakinisumbua hatimaye nafanikiwa kuchukua taji hili hapana siwezi kuamini kwa kile nilichosikia kuwa ndiyo mshindi wa Masters 1000 na kumshinda Roger hakika ni hajabu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents