Burudani

Dela adai amekuwa kama mwalimu wa Kiswahili baada ya cover ya Hello

Muimbaji wa Kenya Adeline Maranga aka Dela aliyewahi kufanya cover ya wimbo wa ‘Hello’ wa Adele amesema kuimba kwa Kiswahili kwenye wimbo huo kumemuongezea umaarufu zaidi na sasa amekuwa kama mwalimu wa lugha hiyo.

14716499_324432134595708_412701504802127872_n

Dela amemuambia mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa amepata comment nyingi kutoka kwa mashabiki ambao wengi wanatamani kujifunza Kiswahili baada ya kuusikia wimbo huo.

“Kuna watu hata ukiangalia comment zao kwenye Youtube wanasema kwamba hawajui Kiswahili lakini sasa wanataka kujifunza Kiswahili au wanasema mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili hapa America na nitawaimbia wanafunzi wenzangu huu wimbo. Pia na mimi nimekuwa mwalimu kwa njia ya Kiswahili,” amesema Dela.

Muimbaji huyo aliwahi kushirikishwa na AY kwenye wimbo wa Asante.

https://youtu.be/0lh2GJwDFfs

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents