Michezo

Dele Alli: Ni bora nitundike daluga kuliko kujiunga Arsenal

Mchezaji wa klabu ya Tottenham Dele Alli amesema ni heri astaafu soka kuliko kuwachezea mahasimu wao wa London kaskazini Arsenal.
Kinda huyo, 20, amefanya makubwa katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu wakati Spurs ikiwani ubingwa wa ligi.

ali1

Uwezo wake uwanjani umemfanya aorodheshwe katika tuzo ya kuwania Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu na amesaidia kikosi chake kuwa juu ya mahasimu wao kwa mara ya kwanza tangu 1995.

Alipoulizwa na mtandao wa Copa90 kuwa, kama angepewa nafasi ya kuchagua Arsenal au kuachana na soka, mchezaji huyo wa zamani wa MK Dons wala hakubabaika kujibu.

“Nitatundika daluga zangu,” alijibu alipoulizwa ajibu kuhusu mazingira hayo, na kuthibitisha kuwa ni namna gani ni mwaminifu White Hart Lane.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents