Michezo

Dele Alli, Paul Clement na Andy Carroll washinda tuzo za EPL

Shirikisho la soka la Uingereza, FA limemtangaza mchezaji bora wa mwezi Januari ambapo Dele Alli anayechezea klabu ya Tottenham Hospurs amefanikiwa kushinda tuzo hiyo.

Dele amehusika katika magoli 6 yaliyofungwa na timu yake katika mexchi tano walizocheza ikiwemo na timu ya Watford, Chelsea, West Bromwich Albion na Manchester City.

Wakati huo huo kocha wa Swansea City, Paul Clement ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi wa ligi hiyo ya Uingereza.

Naye mchezaji wa West Ham United, Andy Carroll ameshinda tuzo ya goli bora la mwezi ambalo alifunga Januari 14 walipocheza na Cristal Palace huku akiyapiku magoli mengine likiwemo la Olivier Giroud la ‘scorpion kick’, Wayne Rooney, Lucas Perez na Marko Arnautovic.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents