Michezo

Denmark yalazimishwa sare na Australia kombe la dunia nchni Urusi

Timu ya taifa ya Denmark imelazimishwa sare ya bao 1 – 1 dhidi Australia mchezo wa kundi C  uliyopigwa dimba la Samara Arena michuano ya kombe la Dunia inayoendelea huko Urusi.

Denmark imefanikiwa kufunga bao lake lakuongoza kupitia kwa kiungo wake  anayekipiga klabu ya Tottenham Hotspur, Christian Dannemann Eriksen kabla Australia haija zinduka na kusawazisha kupitia kwa Jedinak na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya bao 1  –  1.

Mpaka sasa kumepigwa jumla ya mikwaju ya penati 11 kwenye michuano hii ya kombe la dunia 2018 ukilinganisha na ile ya mwaka 2014 ambapo zilikuwa 10 pekee.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Denmark kuongoza kundi C lenye timu za Australia, Ufaransa na Peru kwakujikusanyia jumla ya pointi nne nyuma ya Ufaransa wenye alama tatu na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga hatua ya 16 bora.

Kwenye michuano hiyo ya kombe la dunia mpaka sasa kumeshapigwa jumla ya mikwaju ya penati 11 kwa mwaka huu 2018 ukilinganisha na mwaka 2014 ambapo zilipigwa 10.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents