Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Deontay Wilder aridhia kuzipiga na Anthony Joshua ndani ya Uingereza dau nono latengwa

Promota maarufu, Eddie Hearn amesema kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani Mmarekani, Deontay Wilder amekubali kupigana na Anthony Joshua ndani ya ardhi ya Uingereza.


Bingwa wa uzito wa juu duniani Mmarekani, Deontay Wilder

Hapo awali bingwa huyo wa WBC, Wilder alisita kuingia makubali kwa kuhofia upendelo kwa mpinzani wake Joshua mwenyemikanda ya WBA, IBF na WBO akiamini kuwa atatumia nafasi yake ya uwepo nchini kwao na hivyo kumshinda lakini hatimaye bondia huyo wa uzito wa juu ameridhia kuzipiga hapo Uingereza.


Bingwa wa uzito wa juu duniani Mmarekani, Deontay Wilder

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter bondia huyo mwenye umri wa miaka 32 ameandika kuwa nafasi ipo wazi kwa yeye kupigana nchini Marekani pambano lijalo kwa kutengewa kitita cha dola milioni 50. Wakati hii leo akiwa amekubali ofa yake ya kupigana nchini Uingereza.


He tweeted: “The $50m offer for him to fight me next in the US is still available. Today I even agreed to their offer to fight Joshua next in the UK.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW