Siasa

Dhamana Epa Yawaliza Ndugu

BAADHI ya ndugu na jamaa wa wafanyabiashara wanaotuhumiwa wa wizi wa Sh133 bilioni zinazodaiwa kuchotwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania wameitupia lawama Ofisi ya Uhakiki wa hati miliki za majengo kwa kushindwa kuwapa hati miliki za nyumba zao ili waweze kutimiza masharti ya dhamana kwa ndugu zao.

BAADHI ya ndugu na jamaa wa wafanyabiashara wanaotuhumiwa wa wizi wa Sh133 bilioni zinazodaiwa kuchotwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania wameitupia lawama Ofisi ya Uhakiki wa hati miliki za majengo kwa kushindwa kuwapa hati miliki za nyumba zao ili waweze kutimiza masharti ya dhamana kwa ndugu zao.
Wakizungumza na Gazeti hiyo jana, ndugu hao walisema kuwa ofisi hiyo imekuwa kikazo kikubwa kwa ndugu zao kuendelea kusota rumande. Mpaka sasa ni watuhumiwa wawili kati ya 20 waliotimiza masharti ya dhamana.
Ndugu hao walidai kuwa siku ya kwanza baada ya ndugu zao kufikishwa mahakamani hapo walikwenda katika ofisi hiyo iliyopo katika jengo la Wizara ya Ardhi, lakini wakakuta ofisi hiyo imefungwa hivyo kukwamisha zoezi la kuwadhamini ndugu zao.

Mpaka sasa watuhumiwa 20, kati yao wakiwamo watatu ni wafanyakazi wa BoT wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mbele ya mahakimu tofauti. Kati ya hao watuhumiwa wawili tu ndiyo waliotimiza masharti ya dhamana na tayari wako nje.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi waka wakati tofuati kuanzia wiki iliyipita na kuwekewa masharti magumu ya dhamana ambayo wengi wao wameshindwa kutimiza.

Wtu hao ambao sasa wako mahabusu wanashitakiwa kwa tuhuma mbalimbali zinazohusiana na upotevu wa mabilioni ya shilingia EPA ikiwamo kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu na uzembe katika kusimia taratibu za utoaji fedha BoT.

Karibu maofisa wote wa BoT wameshtakiwa kushiriki katika kashfa hiyo kutokana na uzembe wao katika kusimamia na kudhibiti mwenendo wa fedha kupitia nyadhifa nyadhifa zao. Watuhumiwa hao walikamatwa na kufikishwa mahakamani ili kutekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa wakati akilihutubia Bunge la bajeti mwishoni mwa Agosti mwaka huu, kwamba atakayeshindwa kurejesha fedha anazotuhumiwa kupora ifikapo Oktoba 31, afikishwe mahakmi mara moja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents