Shinda na SIM Account

Dhoruba kubwa yasababisha vifo na kuharibu mali Afrika Kusini

Dhoruba kubwa ya upepo imesababisha vifo vya watu na kuharibu mali mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini, na kusababisha shule mbili kubwa za Krugersdorp na Laerskool Muldersdrif kufungwa kwa muda usiofahamika.

Msemaji wa eneo la Mogale City mjini humo, Nkosana Zali ameuambia mtandao wa Times Live kuwa shule hizo zimefungwa kutokana na uharibifu wa miundombinu iliyosababishwa na dhoruba hilo.

“The buildings are a danger to pupils’ lives,” amesema msemaji huyo. Nyumba takribani 200 zimedaiwa kuharibiwa na watu zaidi ya 15 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Milpark Hospital. Hata hivyo bado idadi ya watu waliofariki katika tukio hilo haijafahamika zaidi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW