Michezo

Di Maria ayaanika maisha yake kupitia ‘tattoo’ (+picha)

Winga hatari wa klabu ya Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Argentina, Angel di Maria ameongeza tattoo nyingine katika mwili wake inayoelezea historia ya maisha yake.

Di Maria amechora tattoo hiyo kwenye mguu wake wakulia huku mchoro huo ukionyesha mazingira yake aliyokulia kama vile nyumba yao ya utotoni iliyopo katika wilaya ya Perdriel, bendera ya taifa lake la Argentina na mpira.

Mchezaji huyo ameonyesha mchoro huo kupitia mtandao wake wa Instagram huku akiandika kuwa historia yangu ipo katika ngozi yangu.

Di Maria huwenda akasherehekea tattoo hiyo mpya endapo timu yake ya Paris Saint-Germain itaifunga Nice katika mchezo wa lgi kuu ya Ufaransa Ligue 1 siku ya Jumapili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents