Diamond Platnumz

Diamond aelekea Marekani wakati collabo yake na J.Martins inakaribia kuiva


Diamond ameamua kutanua mabawa yake zaidi mwaka huu kwa kumshirikisha msanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria, J.Martins. Tayari amesharekodi sehemu zake kwenye wimbo huo kwenye studio za MJ Records chini ya producer Marco Chali.

Habari zinadai kuwa kwa sasa wimbo huo upo kwenye hatua ya final mixing ambapo chorus ya wimbo huo imeimbwa na Diamond na dancer wake Mose Iyobo. Katika kuonesha kuwa bega kwa bega na madancer wake, Diamond ameamua kumpa shavu Mose ambaye ameonesha uwezo mzuri wa kuimba.

J.Martins ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akichukua kozi maalum ya miezi mitatu ya masuala ya utayarishaji, tayari anausubiri wimbo huo ili aingize sauti yake.

Katika hatua nyingine leo Diamond anaelekea mjini Washngton DC nchini Marekani kwaajili ya show. Kwenye safari hiyo Diamond anaenda na madansa wake wote wanne na msemaji wake.

Kwa mujibu wa Power Jams ya East Africa Radio, Diamond atafanya show kwenye mkutano mkubwa unaofanyika Marekani ambao wahudhuriaji wamemtaka akawape burudani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents