Burudani

Diamond akiri mtoto wa Hamisa Mobeto ni wa kwake

Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amekiri kumtambua mtoto AbdulLatif  aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Akiongea katika kipindi cha Leo Tena ya Clouds FM, msanii huyo ameweka bayana ya kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo huyo na mtoto AbdulLatif ni wake ila walikuwa na makubaliano ya kutotangaza katika mitandao.

“Nilifahamiana na Hamisa kabla ya kuwa Miss XXL kipindi kile mwaka 2009 -2010 nilikuwa na mahusiano naye kisha tukaja kuachana. Baada ya kuachana wakati, mimi nikaendelea na maisha yangu na mpaka naanzisha mahusiano yangu na Zari. Shetani akanipitia na tukaanza tena kuwa na mawasiliano ya kimahaba mpaka pale alipopata ujauzito. Nilimuambia mimi ni Baba mwenye familia yangu. Inabidi jambo hili libaki kati yangu mimi na wewe. Sikupenda kuikana Mimba, ni damu yangu na kila siku iendayo kwa Mungu nilikuwa nampatia matumizi,” ameeleza Diamond.

Pia akaongeza kuwa amekuwa akimuhudumia mrembo huyo kutokana na ujauzito huo kwa kuwa anampatia pesa na kumnunulia gari aina ya Rav4. “Kabla ya mtoto kuzaliwa nilitoa shilingi milioni. 7 na laki 5 na nikampeleka hospital ya Private kwa ajili ya kujifungua. Wakati nipo Uingereza nilimuomba Mama yangu aende hospital kumuangalia mtoto, lakini yule mwanamke aliwaita waandishi wakaenda kumrekodi na kumdhalilisha mama yangu,” ameongeza Diamond.

Amesisitiza “Niliporudi kutoka Uingereza nilienda kumuona mwanangu na nikakaa naye sana. Hakuna wakati wowote ambao nilitengeneza mazingira ya kumkataa mtoto. Nashangaa kuona kwenye mitandao wanasema nimemkataa mtoto. Nilichokuwa sitaki ni kuhakikisha mwanamke wangu Zari hatukanwi kwa kuwa hana kosa lolote.” Pia msanii huyo ameomba radhi kwa familia yake na mpenzi wake Zari kwa kosa hilo.

Juni 21, mwaka huu kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM, Diamond aliwahi kukana kuhusika na ujauzito wa mrembo huyo na alimtaka amtaje baba halisi wa mimba hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents