Burudani

Diamond akiwa na mpenzi wake mpya Tanasha, aonesha mamilioni ya fedha aliyovuna Wasafi Festival Mwanza (+video)

Wazungu wanasema ‘HARD WORK WORK PAYS OFF’ na msemo huo unakuja kujidhirisha kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye ameonesha miburungutu ya fedha baada ya kufanya show ya funga mwaka jijini Mwanza ya Wasafi Festival 2018.

Diamond kupitia video aliyoiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, ameonekana kupanga mezani mabunda zaidi ya 10 huku bunda moja likiwa la Dola.

Kwenye video hiyo, Diamond anaonekana akiwa na mpenzi wake mpya Tanasha ambaye yeye muda wote alionekana kuwa bize na  simu.

Diamond na Tanasha bado wapo Mwanza na haijafahamika fedha hizo ni kiasi gani? lakini kwa mahesabu ya haraka haraka ni zaidi ya Milioni 100.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents