Burudani

Diamond akubali Wasafi Festival kudhaminiwa na Alikiba (Audio)

Baada ya Alikiba kuandika ujumbe kwenda kwa Diamond kwamba hataweza kufanya show kupitia Wasafi Festival kutokana na majukumu yake ya kazi huku akiahidi kulidhamini tamasha hilo, Diamond ameibuka na kuzungumzia ishu hiyo.

Hata hiyo ilikuja baada ya Diamond kusema kwamba angependa kumuona Alikiba akifanya show kupitia Wasafi Festival kauli ambayo ilibua msisimko.

Alikiba Jumatano hii alindika

“Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.

Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa. #MofayaByAlikiba#KingKiba,”

Baada ya ujumbe huo, Diamond amerudi upya kupitia post ya Alikiba na kuandika ujumbe ambao unaonyesha huwenda wawili hawa wakawa wamemaliza bifu lao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents