Burudani

Diamond amfariji Zari kufuatia msiba mzito alioupata

Diamond Platnumz ametuma ujumbe wa kumfariji mama watoto wake wake, Zari, kufuatia msiba mzito wa Ivan ambaye ni baba watoto watatu wa Zari.

Diamond akiwa na Zari pamoja na watoto wa marehemu, Ivan. Picha hii ni yazamani

Kumekuwa na mengi yanazungumzwa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu Zari, Ivan na Diamond Platnumz na mengine yamepelekea kuwakera baadhi ya mashabiki wao wa damu.

Diamond ameandika ujumbe wa kumtia moyo Zari The Boss Lady na kuonyesha yupo naye pamoja katika kipindi hicho kigumu anachopitia.

“Natamani ningekukumbatia badala ya kukutumia sms,najua upo kwenye wakati mgumu na ni mpweke, jua kwamba hauko mwenyewe, niko na wewe hapa usiku na mchana,” aliandika Diamond Instagram.

Ivan amefariki dunia Alhamisi hii nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa wiki kadhaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents