AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Diamond ampongeza Joh Makini na WEUSI kwa juhudi zao za kujitangaza kimataifa

Idadi ya wasanii wa Tanzania wanaotuwakilisha kimataifa inazidi kuongezeka, pongezi kwa WEUSI kwa kuamua kujitoa kwa dhati na matunda ya jitihada zao yanaonekana.

11821119_1609709415949187_1581297285_n

Msanii anayeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania nje ya mipaka, Diamond Platnumz amefurahishwa na juhudi za Weusi katika kujitangaza kimataifa, ukizingatia ndio wasanii wa Hip Hop ambao nyimbo zao zimeanza kupewa nafasi kwenye runinga na radio za kimataifa zikiwemo Trace Urban na MTV Base.

Hayo hayakuja hivi hivi, mpaka pale Joh makini na wenzake kwa juhudi zao binafsi walipoamua kuwekeza na kwenda kushoot video ya ‘Nusu Nusu’ Afrika Kusini, na matokeo tayari tumeanza kuyashuhudia.

Diamond

Hit maker wa ‘Nana’ amempongeza Joh Makini na Weusi ambao wamekamilisha kushoot video 2 ikiwemo ile ya collabo yao na rapper AKA wa Afrika Kusini.

Diamond ndiye aliyemleta AKA kwenye Zari All White Party jijini Dar mwezi May mwaka huu, na baada ya AKA kutua ndio Joh alipata nafasi ya kurekodi naye wimbo. Hivyo kwa sehemu kubwa pia Diamond amehusika katika kufanikisha collabo hiyo ambayo soon tutaanza kuiona katika runinga.

Kupitia Instagram hiki ndicho Diamond amekiandika kuhusu Weusi na harakati zao;

“Halaf kweli kesho na Kesho kutwa mtu anakuja anasema Ooh flani freemason ooh mara flani Sjui Anabebwa, ooh sjui Anaroga wakati mtu anaHaso na kujituma 24/7 kila mtu anaona…. mi nakuheshim sana @joh_makini na Team yako nzima ya WEUSI kwa juhudi na Harakati zenu za kilasiku mnazozizidisha…Mwenyez Mungu Aendelee kuwasmamia na Kuwabariki.”

dai kuhusu weusi

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW