Burudani

Zari umenizalia watoto wazuri, ndio maana sikuongelei hovyo kwenye interview – Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz usiku wa kuamkia leo Septemba 23, 2018 amemuandikia mzazi mwenzie Zari ujumbe mzito katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Image result for diamond na zari
Zari na Diamond Platnumz

Diamond amesema ataendelea kumheshimu Zari kwani amemzalia watoto wawili kwake yeye anaona kuwa ni jambo kubwa sana na zawadi iliyo njema.

Hii ni siku muhimu sana kwako mama watoto wangu, Nashukuru kwa kunizawadia watoto wawili wazuri sana na kikubwa zaidi umekuwa mama mwema unawalea watoto vizuri.“amendika Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza hisia zake zaidi.

Niamini mimi, nitaendelea kukuheshimu daima  ndio maana hauji kusikia nikikuzungumzia hovyo kwenye interview zangu ninazofanya, sio hivyo tu hata kuzungumzia chanzo cha mfarakano wa mapenzi yetu kamwe siwezi, watoto wetu tuliojaaliwa ni zawadi tosha kwangu,. Nitaendelea kukupenda, kukuheshimu na kukuchukulia kama dada yangu wa damu.“amemaliza Diamond Platnumz.

Wiki mbili zilizopita Diamond Platnumz alitamka wazi kupitia Wasafi TV kuwa mzazi mwenzie Hamisa Mobetto amesuka mipango ya kutaka kumroga ili achukue baadhi ya mali zake.

SOMA ZAIDI – Unaonekana wewe haushindwi kumuua mama yangu kama unawaza nikupe nyumba – Diamond

Kwa upande mwingine pia Hamisa Mobetto naye amekaririwa mara kadhaa akirusha vijembe kwa familia ya Diamond Platnumz.

Hamisa Mobetto na Zari wote ni wamezaa na Diamond Platnumz lakini mpaka sasa kila mmoja anaishi kivyake .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents