Updates: Diamond asaini mkataba wa show nyingine kubwa ya kimataifa, ni Comoro!!

Wanasema pesa huenda kwenye pesa na mafanikio huvuta mafanikio zaidi. Akiwa hajamaliza hata wiki mbili tangu atoke kwenye tour iliyofanikiwa ya Burundi na Congo, Diamond leo amesaini mkataba wa show nyingine kubwa ya kimataifa.

9f7a436ac3a911e280ff22000a9e2923_7

Kupitia Instagram, Diamond alishare picha inayomuonesha akisaini mkataba wa show huku pembeni akiwepo mtu mwenye asili ya Asia ambaye huenda ndio promoter. Hata hivyo Diamond hakusema ni wapi show itakuwa kwa kuandika: After I did the Uk,Congo,Burundi…guess where next I’ll be headed.”

Na sasa ameweka picha ya mkataba huo unaonesha kuwa show hiyo ni ya nchini Comoro na itafanyika June 22.

0eefc63cc3c011e28dc022000ae90fd2_7

Kabla ya kwenda Burundi na Congo, Diamond alikuwa ametokea Uingereza alikopiga show kwenye miji takriban mitatu. Hivi karibuni pia yeye na Nay wa Mitego walipiga show iliyojaza watu kibao kwenye viwanja vya Dar Live, Mbagala. Jumapili hii pia watakuwa na show nyingine Maisha Club.

Bila wasiwasi, Diamond anaingiza fedha nyingi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW