BurudaniUncategorized

Diamond atangaza kinywaji ambacho kinadhamini Wasafi Festival

Msanii wa muziki na Rais wa WCB, Diamond Platnumz Ijumaa hii ametangaza kinywaji baridi cha pepsi kuwa mdhamini mkuu wa tamasha la Wasafi Festival ambalo litaanza kutimua vumbi November 24 mwaka huu huko mkoani Mtwara.

Muimbaji huyo amemleta mdhamini huyo huku akisubiria wadhamini wengine akiwemo Mofaya.

Naomba Nianze kuwaleta Kwenu Wadhamini wa #WasafiFestival2018 sasa!!!!….Kwanza kabisa naomba Tuwakaribishe Rasmi @Pepsi_tz katika #WasafiFestival2018… Asante sana @Pepsi_tz kwa kuthamini Sanaa yetu… Asante kwa Kuamini katika Vijana… asante kwa Kuamini #WasafiFestiVal208 ….Uwepo wako ndani ya #WasafiFestival2018 Unathamani kubwa sana, na Utaenda Fungua Milango ya Vijana wengi Wenye ndoto ya kufanikiwa kupitia sanaa….. Nasemaje Wadau kuanzia sasa hii ndio soda yetu Rasmi ya #WasafiFestival2018 , na Ukiwa kama Mpenda burudani ya haki naomba kwa Kuwapa shukran kwa Kuisapoti #WasafiFestival2018 kuanzia sasa sie woteTufyekelee mbali visodasoda Vingine….. yani Soda yetu iwe ni Pepsi tu!!!.. na ndugu zake kina Mirinda Nyeusi, 7Up!!!!…😋😋😋😋 Kama Mirinda Nyeusi nishainywaga sana kwa Kujificha ila Round Hii Tutakutana na Pakiti za @DiamondKaranga
#Pepsitz #LiveForNowTZ #LiveForNow
@Pepsi_tz @Pepsi_tz
PEPSI USIIICHEZEE WEWE!!!!!!

Mofaya ni kinywaji cha Alikiba ambacho kilitangaza kulidhamini tamasha hilo mapema wiki iliyopita siku mbili baada ya kuzinduliwa.

Mmoja kati ya wakurugenzi wa WCB, Mkubwa Fella aliiambia Bongo5 kwamba kwa sasa mazungumzo ya Wasafi Festival kudhamini tamasha hilo yanaenda vizuri.

“Kusema kweli mazungumzo yanaenda vizuri sana lakini msije mkaanza maneno msipo waona kwenye show ya kwanza ya Mtwara kwa sababu show tunazo nyingi na wao wanaweza kuanza kuonekana kwenye show nyingine,’ alisema Fella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents