Burudani

Diamond atangaza ujio wa msanii mwingine wa kike WCB ‘naamini wanawake wanaweza, wakiwezeshwa’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB, Diamond Platnumz ametangaza rasmi ujio wa msanii mwingine wa kike kwenye lebo yake.

Diamond amethibitisha hilo kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambapo amesema kuwa anaamini mwanamke akiwezeshwa anaweza.

Nipo mbioni kumtambulisha msanii wa kike (WCB), kwa sababu naamini wanawake wanaweza, wakiwezeshwa,” ameandika Diamond Platnumz .

Kwa sasa lebo ya WCB ina msanii mmoja wa kike, Queen Darleen. Swali ni je, msanii gani wa kike atakayetambulishwa.

Kwa tetesi zilizopo chini ya kapeti, inaelezwa kuwa mtoto wa Mwimbaji wa Taarabu, Khadija Kopa aitwaye Zooccu Kopa (Zochu) ndiye msanii anayetarajiwa kusainiwa. Unaweza ukatazama cover alizowahi kuzifanya msanii huyo

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents