Burudani

Diamond atangaza ujio wa tamasha la Wasafi Festival mwaka huu

Diamond Platnumz ni mfanyabiashara ambaye anatumia kila fursa inayopita mbele yake bila ya kuogopa chochote. Msanii huyo ametangaza ujio wa tamasha kubwa jipya la Wasafi Festival ambalo litafanyika mwaka huu.

Mashabiki wengi wa muziki wamekuwa wakitamani kuona tamasha kama hilo kutoka kwa wasanii hao wa WCB, lakini bahati nzuri kupitia mtandao wa Instagram, Diamond amethibitisha ujio wa tamasha.

“Kama Naiona hiyo #WasafiFestival Huu Mwaka Sijui hata tuanzie Mkoa gani???🙆‍♂️,” ameandika hit maker huyo wa African Beauty.

Hata hivyo Disemba 2016, WCB walifanya matamasha mawili makubwa likiwemo la Wasafi Beach Party lililofanyika Jangwani Sea Breezy jijini Dar es Salaam, na jingine mkoani Iringa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents