Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Diamond atoa povu kwa wanaofuatilia mahusiano yake

Diamond Platnumz ameamua kutema cheche kutokana na watu kufuatilia mahusiano yake kwa ukaribu kila kukicha.

Kupitia mtandao wa Instagram, hit maker huyo wa ‘Hallelujah’ ameonekana kuumizwa na maneno yanayoendelea kuzungumzwa mitandaoni na kuamua kusema kuwa ikifika muda wa kuweka wazi atafanya hivyo kwani hakuna kitakacho mzuia.

Kupitia mtandao huo, Diamond ameandika:

Mara Diamond Kamla Huyu, mara sjui naskia anatembea na Huyu, Mara Ooh sjui inasemakana juzi alikuwa na Huyu…Yani kila Ukiamka limezuka jipya, Utazani yangu ina Sukari au Nakojoa dhahabu?…..Hebu Niacheni kidogo, niko Busy nahangaika kuipeleka Bongo fleva yetu Duniani…. Sijamkaza yoyote, na Sina Mahusiano na Yoyote anaetajwa, na Siku pia Nikimaliza Mahusiano yangu na Alie South na nikawa na Mwengine na ikifikia kuliweka wazi ntaliweka wazi Mwenyewe, Maana hakuna kitachonizuia… ndio kwanza nna miaka 28, Sijaoa na Hata nikioa Naruhusiwa niwe na wake Wanne PERIOD!!!….

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW