Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Diamond atua kwenye mtandao wa mastaa wakubwa duniani

Malengo ya Diamond Platnumz yanazidi kutimia kila kukicha. Moja wapo ni kuhakikisha kuwa jina lake linavuka kutoka kujulikana Afrika na kutambulika kwenye mabara mengine hasa Ulaya na Marekani.

Ikiwa Jumatatu hii ya Octoba 2, ni siku ambayo msanii huyo anasherekea siku yake ya kuzaliwa, taratibu ameanza kupata tobo, mtandao maarufu ambao unaonyesha siku ya kuzaliwa ya mastaa wakubwa duniani, Famous Birthday umempa shavu muimbaji huyo wa Hallelujah.

Mtandao huo umeonyesha kuwa Diamond amezaliwa siku moja na mastaa wengine kama Mahatma Gandhi ambaye ni kiongozi wa kukumbukwa aliyepigania uhuru wa India, Roberto Firmino (mchezaji wa Liverpool), Sting (mwanamuziki wa Rock), Kelly Ripa (mtangazaji wa runinga), Lene Nystrom (mwanamuziki wa Pop) na wengine.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW