Habari

Diamond, Dogo Janja waungana na Watanzania wengine kutoa msaada kwa kijana mwenye kansa (+Video)

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja pamoja na Diamond Platnumz wamekuwa miongoni mwa wasanii wanao toa msaada kwa vijana wengi wenye matatizo. Hii imetokea baada ya wasanii hao kutoa msaada kwa kijana anayeitwa Rajabu mwenye matatizo ya Kansa ya mifupia.

Kijana huyo amepata msaada kwa Wasanii hao akiwa anatakiwa kwenda kutibiwa nchini India, na Dogo Janja ametoa msaada wa shilingi za Kitanzania milioni mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameandika kuwa ” Niliposema nimeumizwa na kijana mwenzangu Rajabu nilimaanisha,nimekabidhi shilingi milioni moja kwa wahusika wanaomuhudumia,sitoi kwa kuwa zimezidi”

Haya ndio maneno ya Dogo Janja.

Mbali na kutoa msaada huo kwa jina huyu mwenye matatizo ya mifupa, siku za hivi karibuni pia aliamua kurudisha fadhila zake kwenye shule aliyosomea kwa kupeleka rangi na mabati kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo. baada ya kutoa msaada huo aliandika haya.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents