Burudani

Diamond, Dully Sykes, Fid Q na wengine kukiwasha Freshers Party Dar

Wasanii wa muziki, Diamond pamoja na team yake nzima ya WCB, Fid Q, Dully Sykes na Christian Bella watafanya show ya nguvu katika Freshers Party 2017 iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwaajili ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo mbalimbali vya mkoani humo.

Show hiyo kwa mara ya kwanza nchini Tanzania itafanyika Jumamosi hii Disemba 2 katika parking ya Mlimani City.

Wanafunzi wengi wanashahuku ya kushuhudia show hiyo ya aina yake kwa kuwa itakuwa imebewa wasanii wakubwa ambao mara nyingi ni radra kuwaona katika show mbalimbali za mashuleni.

RC Makonda alisema show hiyo ina lengo la kuwakaribisha wanafunzi ndani ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na kupeana fursa na utaratibu wa mambo mbalimbali yanayopatikana ndani ya jiji hilo la kibishara.

Alisema kuzungumza na wanafunzi hao kutawafanya watambue ni nini kimewaleta Dar es salaam pamoja kuwa mabalozi wa usalama ndani ya jiji.

Pia alisema katika show hiyo muda mwingi itakuwa ni kwaajili ya burudani ili kuwafanya wanafunzi waburudike zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents