Diamond Platnumz

Diamond kufanya usaili wa kupata watu watakaoonekana kwenye video yake mpya

Akiwa miongoni mwa wasanii wa Tanzania wanaolipwa pesa nyingi zaidi kufanya show, Diamond Platnumz anaweza kufanya lolote ili atoe kitu kizuri.

Mara nyingi auditions za kutafuta mamodel watakaoonekana kwenye video za nyimbo hufanyika nje lakini Diamond ameamua kuonesha njia.

Taarifa za kufanyika kwa usaili huo zimetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole aliyedai kuwa msanii huyo ambaye jina lake halis ni Abdul Naseen amefikia uamuzi huo ili kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.

“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.

Mwendapole alisema video hiyo itafanyika ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya soko ambalo msanii huyo analiangalia kwa sasa. Japo haijuitaja, lakini alisema video hiyo itafanywa na kampuni ya Tanzania.

Kwa upande wake Diamond alisema lengo la kufanya usaili ni kuleta mapinduzi ya kimuziki nchini na pia kutoa ajira kwa vijana wenzie wa kike na kiume.

Hivi karibuni msanii huyo anatarajia kurudi tena nchini Marekani kupiga show nyingine baada ya hivi karibuni kuzikonga nyoyo za mashabiki wake wa Washington DC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents