Burudani ya Michezo Live

Diamond kuileta collabo nyingine na Donald, ya Chris Brown inafuata?

Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini ambapo pamoja na mambo mengine, inaonesha ameenda kushoot video ya collabo yake nyingine na staa wa muziki wa R&B na house nchini humo, Donald.

Hii inakuwa mara ya pili wakali hao wanafanya wimbo pamoja. Mwaka 2015 wawili hao waliachia wimbo uitwao Wangu.

Wote wameweka clip ya video Instagram wakielezea kukutana kwao kwa mara nyingine tena.

“Always nice meeting my south African brother @donaldindenial …..!” ameandika Diamond.

Naye Donald ameandika: The Pride of African Music @diamondplatnumz.”

Wakati huo huo, huenda Diamond akawa anatupa habari kimafumbo kuwa kuna uwezekano wa kumweka Chris Brown kwenye mipango yake ya collabo za baadaye. Akiweka picha ya staa huyo, Diamond ameandika: Nifunge bakuli langu….nikojoe nikalale, Mie bado Mudogo sana…..

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW