BurudaniDiamond Platnumz

Diamond kwenda Nigeria mwezi huu kufanya video mpya, Number 1 imefanya sasa anaombwa collabo na Waghana na Wanaija

Ni ukweli usiopingika kuwa msanii Diamond Platnumz ameendelea kupata mafanikio makubwa kimataifa kupitia hit single yake ya mwaka jana ‘Number 1’ amabayo alikuja kumshirikisha star wa Nigeria Davido katika remix ya wimbo huo.

platnm

Licha ya video ya ‘Number 1 Remix’ kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika Top 10 ya kituo kikubwa cha TV cha kimataifa Trace Urban ya Ufaransa, Diamond amesema kwa sasa amekuwa akipokea maombi kutoka kwa wasanii wa Ghana na Nigeria wote wakitaka kufanya naye Collabo, kitu ambacho zamani yeye ndiye aliyekuwa akihangaika kutafuta connection ya kufanya collabo na wasanii wa huko.

“Ukiangalia saizi nyimbo inafanya vizuri sana Nigeria inafanya vizuri sana Ghana hapa nilipo nina collabo kama tatu naombwa kutoka Ghana watu wanaomba kufanya Collabo na mimi, sio Ghana hadi Nigeria kuna watu wanaoniomba mimi kufanya nyimbo na mimi, wakati haikuwa hivyo before…” Diamond aliiambia E News ya EATV.

Ameongeza kuwa anatarajia kuachia single mpya siku si nyingi ambayo pia itakuwa ni moja ya collabo za kimataifa ambazo amefanya na wasanii mbalimbali. Pamoja na kwamba hajaweka wazi ni wimbo gani anaotarajia kuutoa, lakini baadhi ya wasanii wakubwa ambao ameshafanya nao collabo hadi sasa ni pamoja na Iyanya na D’Banj wote wa Nigeria.

Platnumz ameongeza kuwa mwisho wa mwezi huu anatarajia kusafiri kwenda tena Nigeria kushoot video yake mpya pamoja na kufanya collabo zingine kwaajili ya soko la Afrika kwa ujumla.

“Tarehe 30 kama sikosei nasafiri narudi tena Nigeria naenda kushoot video yangu mpya, ukiacha tu video kuna collabo collabo zangu naenda kuzifanya za kiAfrika. Unajua kuna vitu viwili kuna muziki wa East Afrika na muziki wa Afrika kwa ujumla so lazima uangalie market inafanyaje na we ujue unafanyaje”. Alimaliza Diamond.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents