Burudani

Diamond naye akawa ananiita Simba – Msami

Msanii wa Bongo Flava na Dancer maarufu, Msami ameeleza ulipoanzia utaratibu wa wasanii kujiita Simba jina ambalo Diamond Platnumz amekuwa akilitumia.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa wakati wanaenda kushiriki mashindano ya kudansi yeye na Mose Iyobo walipenda kutumia jina hilo hasa pale wanapokutana na dancer wenye uwezo wa chini zaidi yao.

“I think hata jina la Simba lilianzia kwa mimi na Mose, mimi nilikuwa nakutana na Mose ananiita Simba, namuita yeye Simba that time Diamond alikuwa anacheza lakini sio sana,” ameimbia The Playlist ya Times Fm na kuongeza.

“Diamond ni mtu ambaye alikuwa anakuja kwenye mashindano ya dance. Hata nikienda kufundisha kule Wasafi Mose ananiitaga Simba, Diamond naye akawa ananiita Simba na mimi nikawa namuita Simba mpaka baadae limekuwa kubwa lakini lilivyoleta stori nyingi huwezi kuibuka na kusema utaonekana kuna vitu unahitaji,” amesema Msami.

Msami kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘So Fine’ ambayo amemshirikisha Chemical.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents