Diamond Platnumz

Diamond Platnumz aufungua mwaka 2013 vibaya

Platnumz

Diamond platinum amefungua mwaka vibaya baada ya show yake ya jana pale Maisha Club kumwendea ndivyo sivyo. Usiku wa Wasafi haukwenda kama ulivyokua umepangwa baada ya kutokea fujo kubwa.

Show hiyo ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza baada ya kundi kubwa la vijana wasiojulikana kuanza kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond.

Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi mpiga picha wake Bestizo Mkononi. Kuona hivyo Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.

Vitu vya thamani kama cheni,pete na camera ya Bestizo ya ThisisDiamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond kuharibika.

Source: Sam Misago

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents