Burudani

Diamond Platnumz hakamatiki, atokea kwenye Grammy

Vichwa vya habari  vikubwa Kutoka Kwa Star wa Muziki kutoka Tanzania na barani Afrika kwa ujumla  @diamondplatnumz , baada ya kufanyiwa mahojiano maalumu na waandaaji wa Tuzo kubwa duniani za Muziki GRAMMYs (@recordingacademy )

Kupitia Website yao Pamoja na Kurasa zao za Mitandao ya Kijamii , Grammy wamemuelezea @diamondplatnumz kama mwanamuziki aliyeweza kubadilisha taswira ya Muziki wa Afrika Mashariki Pamoja na kufikia viwango ambavyo ni ndoto ya kila mwanamuziki kufika .

Grammys Pia wamesifu jitahada za Diamond , kuweza Kuongezea Radha za Kiingereza na Kiswahili katika Muziki wa “BongoFleva” kitu kilichofanya aweze kuvuka mipaka na kufanya kazi na Wasanii wakubwa duniani kama vile @omarion , @richforever , @neyo na @aliciakeys .

Tuzo za Grammys ndio Tuzo kubwa zaidi za Muziki Duniani na ndoto ya kila mwanamuziki ! Hivyo kitendo cha waandaaji wa Tuzo hizi kumzunguzia na kumpa heshima @diamondplatnumz , ni ishara nzuri kwa Muziki wa Afrika Mashariki .

Je, unadhani Diamond ataweza kuandika Historia na kuleta Tuzo ya Grammy Tanzania ?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents