Tupo Nawe

Diamond Platnumz kuachia ngoma mpya kesho

Diamond na Raqey wakichagua picha ya kutumia kwenye cover ya wimbo wake mpya

Baada ya miezi kadhaa ya ukimya bila track mpya hewani hatimaye staa wa ‘Mawazo’ Diamond Platnumz kesho anatarajia kuachia wimbo wake mpya.

Ngoma hiyo ameipa jina la ‘Nataka Kulewa’ ambayo imefanywa na producer wa AM Records, Manecky.

Kupitia website yake, Diamond ameshare kwa mashabiki wake picha za utengenezaji wa cover ya ngoma hiyo uliosiomiwa na Raqey Mohamed wa I-View Media kampuni ambayo inamsimamia.

Kuhusu mipango ya video aliyoifanyia usaili wa models wiki kadhaa zilizopita Raqey amesema bado wanashughulikia permit na hivi karibuni alikuwa Dubai kwaajili ya kuweka mambo sawa.

Hizi ni baadhi ya picha hizo. Picha kwa hisani ya thisisdiamond.com

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW