Burudani

Diamond, Rayvanny wafungiwa na BASATA kufanya show ndani na nje ya nchi, Wasafi Festival yapigwa STOP kuendelea (+audio)

Baraza la Sanaa Taifa  (BASATA) limewafungia  wanamuziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Diamond Platnumz na Rayvanny  kutofanya show ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana.

Taarifa  iliyotolewa leo Desemba 18, 2018 na BASATA,  imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Kwa upande mwingine, BASATA  wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linalotarajiwa kufanyika nje ya nchi baada ya kuzunguuka kwenye baadhi ya mikoa hapa Tanzania.

Imeelezwa kuwa wimbo wa Mwanza ndio uliowaingiza matatani, baada ya wasanii hao wikiendi iliyopita kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi Festival jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents