Wema Sepetu

Diamond si yupo na Zari au? Sidhani kama amemind mimi kufanya kazi na Wema – Ommy Dimpoz

Kwa imani ya watu wengi Ommy Dimpoz ana kesi ya kujibu kwa Diamond Platnumz baada ya kumtumia Wema Sepetu kwenye video ya wimbo wake mpya Wanjera.

Ommy na wema

Hata hivyo Ommy amesema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo licha ya Diamond kutoandika chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.

Ommy amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa huenda shughuli nyingi za Diamond ndio sababu iliyomfanya akashindwa kuandika chochote kuhusiana na Wanjera.

“Labda hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au? Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents