Burudani

Diana amkana Aslay ‘mbona huyo mtu simjui’

Muigizaji wa filamu Diana Kimaro amekanusha kutoka kimapenzi ya muimbaji Aslay baada ya kuonekana kuwa karibu zaidi katika siku hizi za usoni.

https://www.instagram.com/p/BkQbDlYB2aS/?taken-by=aslayisihaka

Wawili hao kila mmoja amekuwa akipost picha ya mwenzake na kutoa ujumbe ambao unatafsiriwa na wengi kwamba wawili hao wako kwenye mapenzi mazito.

Akiongea katika kipindi cha U heard cha Clouds FM, Diana amedai hamjui Aslay huku akienda mbali zaidi kwa kudai kwa sasa hayupo kwenye mahusiano.

“Mimi sina mahusiano na mtu yeyeto, mbona huyo mtu simjui,” alisema mrembo huyo ambaye ni mara chache sana kuonekana akijiachia na wanaume.

Aslay ambaye hivi karibuni ameachana na mama watoto wake, hajazungumza chochote kuhusiana na picha zake zinazosambaa mtandaoni na mrembo huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents