Burudani

Diddy aongoza orodha ya matajiri wa Hip Hop

P Diddy hakamatiki kwa mkwanja wake. Forbes imemtaja rapper huyo kuwa na utajiri wa dola milioni 820 na kumfanya kuendelea kuongoza orodha ya mastaa watano wa Hip Hop wenye mkwanja mrefu zaidi duniani.

Rapper huyo ameendelea kuingiza fedha hizo kutokana na biashara zake nyingi ikiwemo Cîroc Vodka, Revolt TV, na ziara yake iliyoanza mwaka jana ya “Bad Boy Family Reunion Tour.” Naye Jay Z anashika nafasi ya pili katika orodha hiyo akiwa na kiasi cha dola milioni 810.

Utajiri huo wa Jay Z umetokana na kampuni zake za Tidal, Roc Nation, Roc Nation Sports na dili nyingine kupitia filamu anazofanya kupitia kampuni ya Weinstein Company. Katika kusherehekea hilo, Diddy kupitia mtandao wa Instagram, ameweka picha yake akiwa na Jay Z na kuandika, “We push each other… We inspire each other… #BlackExcellence.”

Wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni Dr. Dre ($740) million, Birdman ($110) million na Drake ($90) million. Kwa mwaka jana orodha hiyo iliongozwa na Diddy akifuatiwa na Dr. Dre, Jay Z, Birdman na Drake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents