Burudani

Diddy kumrudisha Notorious B.I.G. (picha)

Baada ya kutoka filamu ya ‘All Eyes On Me’ iliyokuwa ikielezea maisha ya rapa Tupac Shakur, sasa macho tuelekeze kwenye ‘Can’t Stop Won’t Stop’.

‘Can’t Stop Won’t Stop’ ni filamu ya rapa na mfanyabiashara Sean ‘Diddy’ Combs, itayoonyesha matukio mbalimbali ya msanii huyo anayemiliki lebo ya Bad Boy.

Moja ya vitu vinavyotarajiwa kuonekana ni pamoja na hustle zake alizozifanya mpaka kutoboa pamoja na harakati za kuwasaidia wasanii kama Notorious B.I.G.

Kwa saa za Afrika Mashariki, filamu hiyo imezinduliwa alfajiri ya leo na imehudhuriwa na mastaa kadha wakiwemo aliofanya nao kazi kama Lil Kim, Usher Raymond, Dr Dre na wengine.

Siku ya Jumapili ndio rasmi ‘Can’t Stop Won’t Stop’ itaanza kupatikana kwa mfumo wa Apple Music.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents