BurudaniUncategorized

Diddy na Dj Khaled watarajiwa kuungana pamoja kwenye hili

Rapper P Diddy na Dj Khaled wanatarajia kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuukuza muziki wa Hip Hop.

Wasanii hao wapo katika mazungumzo na kituo cha runinga cha Fox kwa ajili ya kuwa majaji wa kipindi cha kutafuta wasanii wa Hip Hop wenye vipaji.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umesema majaji wanne ndio wanatakiwa katika kipindi hicho akiwemo mmoja ambaye ni rapper, mtayarishaji wa muziki, mwandishi wa nyimbo na mtu wa kudansi. Miongoni mwa watu hao wanne waliotajwa ni Diddy na Khaled.

Kipindi hicho ambacho kitakuwa kinarushwa na kituo hicho cha Fox kimepewa jina la ‘The Four’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents