Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Didier Deschamps awashusha presha Wafaransa kuhusu majeraha ya Olivier Giroud

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema kuwa mshambuliaji wake Olivier Giroud atapata unafuu mapema tayari kwajili ya mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia dhidi ya siku ya Jumamosi.

Straika huyo wa klabu ya Chelsea amepata majeraha maeneo ya paji lake la uso wakati alipo gongana vichwa na beki, Matt Miazga wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya taifa dhidi ya Marekani mchezo wa kirafiki uliyomalizika kwa matokeo ya bao 1 – 1.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alipata matibabu ya huduma ya kwanza kwa zaidi ya dakika tano uwanjani kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Ousmane Dembele.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW