Michezo

Diego Costa aachwa katika timu ya taifa ya Hispania

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania katika michezo miwili ya wiki ijayo. Kocha Vicent Del Bosque amesema hajafurahishwa na tabia ya mchezaji huyo aliyoifanya dhidi ya Arsenal.

diego2-634x360

Hispania inahitaji point moja tu ili kufuzu katika michuano ya mataifa ya Ulaya na wiki ijayo itapambana na Luxembourg na Ukraine katika michezo yake ya mwisho ya kundi.

Mshambuliaji wa Juventus ambaye anafanya vizuri kwa sasa, Alvaro Morata ameitwa kikosini na anatarajiwa kushika nafasi ya Diego Costa katika kikosi cha kwanza.

Wachezaji wenza watatu wa Chelsea Cesar Azzpilicueta, Cesc Fabregas na Pedro Rodriguez wote wameitwa sambamba na Carzola wa Arsenal na wachezaji wawili wa Manchester United, David De Gea na Juan Mata huku David Silva wa Manchester City akikamilisha orodha ya wachezaji 23.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents