Michezo

Dili la Alexis Sanchez lamfanya kukosa vipimo vya utumiaji wa dawa za kulevya

Kuna uwezekano kwamba Arsenal na Alexis Sanchez wakafunguliwa mashtaka na FA baada ya Sanchez kukosa vipimo vya kama anatumia madawa ya kulevya vilivyo fanyika siku aliyojiunga na Man United.

Kutokana na taarifa walizotoa The Sun ni kwamba kwa sasa Shirika la Kupinga utumiaji wa dawa za kulevya la Uingereza linachunguza madai ya Arsenal ya kushindwa kuwaambia FA kuwa mchezaji huyo hakuwepo mazoezini siku ya Jumatatu.

Shirika hilo la FA walienda katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal na Sanchez alikuwa katika orodha ya majina ya wachezaji ambao wanatakiwa kufanyiwa vipimo.
Lakini Arsenal wao wanatakiwa kuwajulisha FA juu ya mabadiliko yoyote kwenye ratiba zao za mazoezi kila siku inasemekana kuwa walipuuza kutokuwepo kwa Sanchez katika siku hiyo.

Sanchez hatozuiwa kucheza mechi yake ya kwanza Manchester United dhidi ya Yeovil katika Kombe la FA usiku wa leo. Arsenal watakumbwa na mashtaka kama FA hawatokubali maelezo yao kwa

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents