Habari

Dilma Rousseff apigwa chini rasmi Urais nchini Brazil

Aliyekuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Brazili, Dilma Rousseff ameondolewa rasmi kwenye kiti chake hicho baada ya kupigiwa kura na baraza la senate za kutokuwa na imani naye.

Rousseff

Bi. Rousseff aliondolewa kwenye kiti hicho cha Urais baada ya kufanya udanganyifu kwenye bajeti ya nchi hiyo kitendo kilichomfanya kuondolewa kwenye nafasi hiyo mwezi Mei mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa kwa muda na aliyekuwa makamu wake Michel Temer huku zikisubiriwa kura za baraza la sanatee ambazo ndizo zingeamua hatima ya rais huyo.

Kwa mujibu wa kura zilizopigwa na senate ya baraza hilo zimeonyesha kuwa asilimia 61 zimemtaka Bi. Rousseff kuondoka madarakani huku asilimia 20 zikipinga uamuzi huo. Baada ya uamuzi huo wa baraza la senate Bi. Rousseff amewashutumu wote waliopiga kura kuwa hawakutenda haki kwa mwanamke asiye na hatia na wamehusika katika mapinduzi ya kisiasa.

Wakati huo huo, aliyekuwa kaimu wa kiti hicho Michel Temer alitangazwa kuwa rais wa nchi hiyo mpaka ifikapo mwaka 2019 ambapo utafanyika uchaguzi mkuu. Akiongea na wananchi kwa njia ya Televisheni baada ya uteuzi huo, Temer ametoa wito watu wote kuungana pamoja na kusema kuwa kuondolewa madarakani kwa Bi. Rousseff kumemaliza miezi kadhaa ya mashaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents