Soka saa 24!

Director wa video ya Camp Mulla ‘Fresh All Day’ kuendesha The Countdown ya Choice FM

Andrew Macharia ni mkenya mwenye umri wa miaka 23. Amekulia Los Angeles, Marekani lakini miezi sita iliyopita amerejea nchini mwake Kenya. Atasikika leo kwenye kipindi cha The Countdown ya Choice FM.

The Countdown huruka kuanzia saa tisa mchana hadi za 11 jioni. Ni kipindi cha kila wiki ambacho huwa na mkusanyiko wa nyimbo 20 bora zilizochaguliwa kwa mapenzi yake mtu maarufu kwenye maeneo mbalimbali husasan katika tasnia ya burudani.

Hucheza nyimbo 20 zilizochaguliwa na mtangazaji wa wiki husika. Nyimbo hizo huzichagua mwenyewe kulingana na muziki anaopenda kuusikiliza kila siku. Hizo huwa ni nyimbo zinazotafsiri wajihi wao pamoja na nyimbo ambazo ziliwasaidia katika vipindi mbalimbali vya maisha yao.

Andrew amesomea masuala ya utengenezaji filamu na video za muziki. Akiwa kama muongozaji wa video, Andy ameshafanya kazi na makampuni makubwa na label kubwa kama Universal Music Group, Warner Bros & Sony Music ambapo ameongoza video za wasanii wakubwa wakiwemo Frankie J, Julian Write, Jasmine Villegas na Young Jeezy.

tumblr_lxwv5stJgv1qc6bdco1_1280

Andy amefanya pia video ya Camp Mulla Fresh All Day, 25flow ya Bamboo, Money Lover ya Sauti, Paradise ya Kanja na zingine na kwa sasa yupo Tanzania kufanya video ya Closer ya Vanessa Mdee.

Leo director huyo mwenye umri mdogo atawapa wasikilizaji wa The Countdown ladha ya muziki anaoupenda. The Countdown hutayarishwa na Maribeth Vuhahulla ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds TV.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW