Aisee DSTV!
SwahiliFix

Dirisha la usajili Uingereza lafunguliwa, Sanchez mikononi mwa juventus na Inter milan, Umited hatiani kumkosa Sancho, Tottenham wajipanga kumrudisha Bale, na wengine sokoni

Dirisha la usajili Uingereza lafunguliwa, Sanchez mikononi mwa juventus na Inter milan, Umited hatiani kumkosa Sancho, Tottenham wajipanga kumrudisha Bale, na wengine sokoni

Juventus wameanza mashauriano na Manchester United kumhusu kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez, 30, ambaye amehusishwa na Inter Milan.(Independent). Manchester United wanamawamezea mate wachezaji mahiri wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, na Patrick Van Aanholt, 28. (Sun)

Chelsea wanapanga kumuongezea mkataba wa mkopo wa Gonzalo Higuain kisha wamregeshe mshambuliaji huyo wa miaka 31 Juventus baada ya fainali ya ligi ya Europa. (Mail)

Gonzalo HiguainHaki miliki ya pichaEPA

Mshambuliaji Crystal Palace Wilfried Zaha(26) amekiambia klabu chakekuwa anataka kuondoka msimu huu wa joto ili kujiunga na soka ya ligi ya mabingwa. Huenda Eagles wakaitisha pauni milioni £80m kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast. (Mail)

Wilfried ZahaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWilfried Zaha

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri mesema ataondoka Stamford Bridge hata akishinda ligi ya Europa- Roma na AC Milan huenda wakatafuta huduma za Mtaliano huyo, huku Blues wakitarajiwa kumsaka meneja wa Watford Javi Gracia. (Express)

Chelsea watatoa uamuzi kuhusu hatma ya Sarri kama kocha mkuu baada ya fainali ya ligi ya Europa ambapo watakipiga dhidi ya Arsenal Mei 29. (Telegraph)

Maurizio SarriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaurizio Sarri

Manchester United wanakaribia kumsajili winga wa kimataifa wa Wales na Swansea Daniel James, 21, licha ya tetesi kuwa huenda wakamkosa winga wa kimataifa wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (London Evening Standard)

Real Madrid watawaachilia hadi wachezaji 14 msimu huu wa joto, huku with mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Gareth Bale, 29, Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, na mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia James Rodriguez, 27, wakitarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji hao. (Marca)

Gareth BaleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGareth Bale

Tottenham imesitisha mazungumzo ya uhamisho wa wachezaji wake wa timu ya kwanza hadi baada ya fainali ligi ya Mabingwa itakayochezwa June mosi. (London Evening Standard)

Hatahivyo Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyofuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Ujerumani na Bayer Leverkusen Julian Brandt, 23. (Mail)

Jose Mourinho anadai kuwa meneja akijifanya ‘mtu mzuri ‘ huenda akageuka kuwa ‘kikaragosi’ katika ujumbe wake kwa meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer. (Talksport)

Jose MourinhoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeneja wa zamani wa Manchester United ,Jose Mourinho

West Brom watafanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Brighton Chris Hughton wiki ijayo katika harakati za kumshawishi arejee katika usamamizi wa klabu hiyo. (Telegraph)

Barcelona wanaamini kuwa watamsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28, kutoka Atletico Madrid msimu huu, licha ya kuwa Paris St-Germain pia wanamsaka nyota huyo .(London Evening Standard)

Griezmann hatachukua nafasi ya ya nyota wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho katika klabu ya Barcelona, kwa mujibu wa wa meneja wa mchezaji huyo raia wa Brazili. (Sky Sports)

Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPhilippe Coutinho

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW