Burudani

Ditto na Amini wapongezwa kwa utunzi wa Hello Hello Tanzania

Kama unaupenda wimbo wa ‘Hello Hello’ Tanzania ambao umetoka kuwa anthem ya uzalendo kwaajili ya Clouds FM tu na kuwa anthem ya kampeni ya uzalendo na mapenzi kwa Muungano wa Tanzania nchi nzima, basi hauko peke yako.

1507556_10202614047385589_543764457_n
Ditto

Wimbo huo uliombwa na wasanii 50 kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika jana Jumamosi jijini Dar es Salaam, umesifiwa na viongozi wengi na wasanii mbalimbali nchini. Sifa hata hivyo zimewaendelea waandishi wa wimbo huo, Lameck Ditto na Amini wa THT. Hizi ni baadhi ya tweets zinazowapongeza.

Fid Q

Hongereni sana kwa uandishi mzuri wa Hello Tanzania.. Hakika mmetengeneza historia! kila la heri kwenye kazi zenu @Lameckditto @aminitz

Hussein M Bashe

@Lameckditto @aminitz Hongereni sana kwa Hello Hello Tz ,God bless All na Artist

Ummy Mwalimu
“@Lameckditto: Hello Hello Tanzania pia niliuandika kwa kushirikiana Na @aminitz”>>Hongera sn. Kazi nzuri sana;-)

Mwamvita Makamba

Hello Hello #Tanzania – Hello Hello Mapenzi ya dhati ! Nanyoosha mikono yangu juu , naisifu nchi yangu maarufu! #TanzaniaAt50, @Lameckditto @aminitz hongereni sana !

Uncle Fafi ‏@Tanganyikan

@Lameckditto Bonge ya wimbo kaka mtaingia kwenye historia kama moja ya watunzi wa wimbo bora wa kizalendo. @aminitz

January Makamba ‏

Hello Hello Tanzania! #Goosebumps

Nchakalih

Mama kaupenda huu wimbo…standing ovation!!! Now please….haki za wasanii zipewe umuhimu wake

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents