Burudani

Diva ashangazwa na maamuzi ya BASATA ‘unafungia msanii badala ya wimbo?’ (+video)

Mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds FM, Diva The Bawse ameshangazwa na baadhi ya maamuzi yanayotolewa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) dhidi ya wasanii wa muziki ambao nyimbo zao zinakiuka maadili ya mtanzania.

Akizungumza na Bongo5, Diva amesema kuwa kitendo cha BASATA kufungia msanii badala ya nyimbo husika ni kibaya kwa sababu wasanii wengi hawana kazi nyingine zaidi ya muziki na wanautegemea kutunza familia zao.

Akitoa ushauri kwa BASATA, Diva amesema kuwa huu ni muda wa Baraza hilo kutambua kuwa ni karne ya 21 na dunia inaenda kasi ni vyema BASATA wakakaa pamoja na wasanii kuangalia namna ya kukuza muziki wetu kwani kwa sasa muziki wa Bongo Fleva unafanya vizuri barani Afrika.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents