Burudani

Diva ataka sakata la unyanyasaji kingono linalomkabili R. Kelly lihamie Bongo, adai mastaa wengi wanafanya ufusika

Mtangazaji wa kituo cha Radio cha Clouds FM, Diva The Bawse ameingilia kati sakata la unyanyasaji kingono linalomkabili msanii nguli wa muziki duniani R. Kelly kwa kutaka sakata hilo lihamie Tanzania.

Diva na R. Kelly

Diva The Bawse amesema kuwa mastaa wengi duniani wanafanya maovu ambayo watu wengi hawayaoni, hivyo ni vyema kukaandaliwa vipindi vya runinga ambavyo vitawahoji watu waliowahi kunyanyaswa kingono.

Nimeangalia #survivingrkelly toka juzi sijashangaa sana kiukweli zaidi ya kuumia. Tatizo liko kote. Kwa wazazi hasa. watu wengi ambao ni wanaitwa role model duniani watu maarufu wengi ni wachafu sana. Sana sana sana. Hata hapa Tanzania wapo zikiruhusiwa docuseries kama hizi tutasikia mengi sana na kuna hata watasema mtu anasingiziwa ili achafuliwe sababu pia fans hawa nao bendera fata upepo sana. Kwanza ndio wanapenda mambo ya ajabu .. So mejiuliza all the time ilikuwaje wakawa kimya? Na wasichana nao wakiona watu maarufu shobo nyingi sana zinakuwa … ndio matokeo kama haya . Very sad … as a woman i was truely hurt kwakweli. Tena hakunaga role model jaman watu hawako kama mnavyowafikiria. Huwa nakaa mbali sana na mwanaume anaenyanyasa mwanamke kwa njia yoyote ile .. awe rafik awe nani nakaa mbali …very heartless. Huwa i distance myself kabisa. The Love i have for Rkelly and his Music … im in pain . Na mauzo yake yameongezeka to 15% unaambiwa …. yan he is on top right now after the docu series. Smh …. wish hizi nazo zitokee Tanzania wanawake wawe free kuelezea wanavyoface kwa so called Role model mnaweza choka mshangae.. shame man!! The fact that uchunguzi umeanza na system ya america ime take action ngoja tuone ukweli ni upi. Ila wanaume jaman .. hii jamii . Watu kama hawa wamejaa …ila wuld luv to hear his side of the story kwakwel duh! Sad Gosh!,“ameandika Diva kwenye ukurasa wake wa Instagram.

R. Kelly kwa sasa anaandamwa na wanaharakati mitandaoni kwa kashfa ya ngono, baada ya Documentary ya Surviging R. Kelly kuanza kurushwa na kituo cha LifeTime.

Kwenye documentary hiyo, wamehojiwa wanawake wote ambao miaka ya nyuma walishawahi kunyanyaswa kingono.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents