Burudani

Diva atoa darasa huru kwa Watanzania wanaolalamika ‘vyuma vimekaza’ (video)

Mtangazaji wa kituo cha Redio Clouds FM, Diva ametoa darasa huru kwa Watanzania wanaolalamika kuwa vyuma vimekaza ambapo kwa upande wake amesema kuwa yeye maisha yake yapo vizuri kama ilivyokuwa zamani.

Akizungumza na Bongo5 amedai kuwa watu wengi hususani wanawake wanaolalamika vyuma kukaza ni wale ambao zamani walizoea kuhongwa lakini kwa wale wanaofanyakazi halali kama yeye haoni tofauti yoyote maisha ya sasa na ya zamani.

Akitoa ushauri amesema huu ni muda kwa watanzania kujifunza kutumia hela vizuri kwa kuzingatia matumizi muhimu na kuacha matumizi yasiyo na umuhimu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents