Shinda na SIM Account

Diva hana kinyongo na Amber Lulu kumchukua Prezzo

Msanii wa muziki Bongo na video vixen, Amber Lulu amesema Diva hana shida wala hajawai kuonyesha kuchukizwa na yeye kuwa katika mahusiano na Prezzo.

Penzi la Prezzo na Diva lilishamiri mwaka 2013 kabla ya kuja kutengana na sasa rapper huyo kutoka nchini Kenya anatoka na Amber Lulu.

Amber Lulu ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa yeye na Diva wapo sawa na mara kadhaa wamekuwa wakikutana na kuzungumza.

“Hapana hajawahi kabisa na juzi nilikuwa naye yupo fresh, nafikiri hivyo ni vitu vya zamani kwa hiyo ana maisha yake na Heri Muziki, kwa hiyo maisha ni mengine na yamebadilika hivyo hamna kumaindiana,” amesema Amber Lulu.

Uwepo wa penzi la Prezzo na Amber Lulu kulianza kuripotiwa katika vyombo vya habari na mitandao October mwaka jana, 2017.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW